MTU mmoja aliyedaiwa kuwa ni daktari wa
jijini Mwanza, Raymond Simion (36) amekutwa amekufa ndani ya chumba
kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ ijulikanayo kwa jina la Nesta
iliyopo Ubungo NHC wilayani Kinondoni jijini Dar.
Taarifa kutoka katika gesti hiyo
zinasema marehemu alijiorodhesha kwenye kitabu cha wageni kuwa ni
daktari wa Hosptali ya Nyamagana jijini Mwanza na alikuja Dar kikazi
kwa muda wa wiki moja. Mauti yalimkuta akiwa na siku mbili tu tangu
alipowasili.
Mmoja wa wahudumu wa gesti hiyo ambaye
hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kuwa, daktari huyo alifika
katika gesti hiyo Jumapili ya Mei 4, mwaka huu na kuchukua chumba namba
102.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Uwazi lilifanikiwa kufika katika eneo la
tukio na kufanya mahojiano na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo
NHC, Amani Sizian ambaye alisema taarifa ya kifo cha daktari huyo
aliipokea saa 9: 03 alasiri ya siku ya tukio ambapo mhudumu wa gesti
hiyo ndiye aliyempigia simu kumjulisha.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa
mhudumu huyo alimweleza kwamba marehemu baada ya kuchukua chumba
Jumapili alitoka na kurudi saa 3:00 usiku ambapo alilala, lakini kesho
yake hakuonekana kutoka.
“Mhudumu aliniambia kuwa baada ya
kutomwona asubuhi, hawakumfuatilia hadi ilipofika saa 9:00 alasiri
ambapo walikwenda kumchungulia chumbani kwake na kumwona katika hali ya
kutokuwa hai.
“Ilibidi niende. Nilipofika tukakuta mlango umefungwa kwa ndani.
“Ilibidi niende. Nilipofika tukakuta mlango umefungwa kwa ndani.
Katika kumchungulia tulimwona mtu huyo
akiwa amekaa kitandani bila kujigeuza jambo lililonifanya nipige simu
polisi ambao walifika na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amefariki
dunia,” alisema mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa, katika chumba hicho
alichofia mteja huyo, kulikutwa mabomba mawili ya sindano ambapo moja
lilikwishatumika, pia kulikuwa na mifuko miwili yenye nguo na begi moja.
Polisi waliuchukua mwili na kuupeleka
Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hata hivyo, ndugu wa marehemu walipatikana
na mwili kufanyiwa uchunguzi na daktari kisha kuuchukua na kuusafirisha
kwenda Mwanza kwa mazishi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,
ACP Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema:
“Marehemu alikutwa na mabomba mawili ya sindano, moja lilishatumika na
lilikuwa na masalia ya damu. Pia kulikuwa na kete moja ya vitu
vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
0 comments:
Post a Comment