Msanii wa filamu Bongo, Halima Yahya ‘Davina’.
SHEREHE ya bethidei ya msanii wa filamu Vivian Minza ambaye ni shosti
wa Halima Yahya ‘Davina’ iliyofanyika Mei 1, mwaka huu imedaiwa kuwa
ndiyo chanzo cha kuvunja urafiki wa wawili hao.
Imeelezwa kuwa kutofautiana kwao ni Davina kutokwenda katika sherehe
hiyo, ili kujiridhisha na madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Davina,
akafunguka:
“Mwenzangu kweli kanichunia lakini najua yataisha tu, sababu ni
kutokwenda kwenye sherehe yake ya kuzaliwa kwani yeye huwa anajitoa sana
kwangu, siku hiyo nilikuwa naumwa sana,” alisema Davina.
0 comments:
Post a Comment