Tuesday 13 May 2014

UN yalaaani shambulizi Somalia

...

130318120712_somalia_mogadiscio_blast_18032013_304x171_reuters_a4076.jpg


Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi baya sana la kujitoa mhanga lililotokea eneo la Kati mwa Somalia Jumatatu.
Taarifa kutoka kwa Muungano wa Afrika imesema kuwa watu 19 walifariki katika shambulizi hilo lililotokea mjini
Baidoa mnamo Jumatatu.
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, alisema kuwa alishtushwa sana na ukubwa wa mlipuko huo, na kuwataka wale waliotekeleza shambulizi hilo kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mji wa Baidoa ulikombolewa na serikali kwa usaidizi wa wanajeshi wa Muungano wa Afrika kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab miaka miwili iliyopita.CHANZO BBC
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger