WAMEANZA! Tabia ya staa wa sinema za
Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ ya kutojumuika na wenzake
kwenye matukio ya kijamii hasa matatizo inadaiwa kuwakera Klabu ya Bongo
Movie Unity hivyo kuandaa kikao maalum cha kumkanya.
Habari kutoka kwa chanzo chetu makini,
zilidai kwamba malalamiko hayo ya kuwa Lulu amekuwa mzito kuhudhuria
shughuli za wenziye kama misiba au hata sherehe zilianza tangu alipotoka
gerezani Segerea, Dar.
Ilisemekana kwamba kilichosababisha
viongozi wa Bongo Muvi kukasirishwa na kuamua kumweka kikao ili kumsema,
ni kwamba ipo siku naye yatamfika.
Baada ya kuzinyaka ‘niuzi’ hizo
motomoto, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mwenyekiti wa Bongo Movie,
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye alikiri kuwepo kwa ishu hiyo ili
kumuonya kwa tabia yake hiyo kwa kuwa yeye bado mdogo.
Alisema Lulu anatakiwa afuate nyayo za
wakubwa zake ambao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali kwa
kuwa ipo siku naye yatamfika.
“Lulu ni mtoto mdogo, hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda.
“Lulu ni mtoto mdogo, hatushindi kwa lolote, lazima tumwambie ukweli kuhusu dunia ilivyo na maisha yanavyokwenda.
“Sisi kama Bongo Movie tuna kawaida ya
kuhudhuria shughuli za wenzetu pale inapobidi lakini kama mtu anakuwa na
udhuru huwa anatoa taarifa lakini yeye hana kawaida hiyo, anajiona
amekamilika.
“Naaamini ipo siku na yeye yatamfika kwa
kuwa mitihani ni kawaida kwa binadamu, sidhani kama mtu atajitokeza na
kumuunga mkono kwa tabia hiyo na siyo yeye tu anayejitenga, wapo na
wengine wengi lakini yeye bado ni mdogo kwetu huenda hajui alitendalo
ndiyo maana tunataka tumfunze jinsi ya kuishi na watu,” alisema Steve.
Kwa upande wake Lulu alipotafutwa na
kuulizwa juu ya jambo hilo hakuonesha mshtuko bali aliwaka: “Huyo
aliyesema hivyo atajijua mwenyewe mimi sina shughuli na mtu, aachane na
mimi.”
0 comments:
Post a Comment