Wednesday 14 May 2014

HOMA YA DENGUE YATIKISA BUNGE-MAKINDA ANENA

...



SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amemtaka Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kebwe Stephen Kebwe kutoa kauli ya serikali juu ya ugonjwa wa Dengu, ambao umetikisa nchi kwa sasa.
Naibu Waziri Kebwe amesimama na kusema kuanzia ugonjwa huu ulipobainika Januari hadi Mei mwaka huu, jumla ya wagonjwa 458 wameripotiwa na watatu kati yao wamepoteza maisha.
Alisema katika jiji la Dar es Salaam, jumla ya wagonjwa 60 wamelazwa hadi sasa katika hospitali za Mwananyamala, Temeke na Ilala. Aidha amesema pia kuwa nchi jirani za Msumbiji na Kenya nazo zimeripotiwa kuwa na wagonjwa wa ugonjwa huo, akisema mjini Mombasa kuna wagonjwa 30 huku Msumbiji kukiwa na wagonjwa 100.
Waziri amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), jumla ya ripoti 500 hutolewa kuhusiana na ugonjwa huu katika nchi mbalimbali duniani na kwamba kati ya wagonjwa watano hadi 500,000 hulazwa.
Katika Afrika, Naibu Waziri Kebwe alisema nchi 34 zimeripotiwa kuwa na ugonjwa huu aliosema unasababishwa na pepo.
Dalili
Alizitaja dalili zake kuwa ni zinazofanana na zile za ugonjwa wa Malaria, ikiwemo homa, kuumwa kichwa na uchovu na hivyo kutoa wito kwa wananchi kwenda kupima mara tu wanapoona dalili hizo.
Aina za Dengu
Alitaja aina tatu za Dengu akiitaja ya kwanza kuwa ni hii ya kawaida ambayo kiasi cha 90% ya wagonjwa wake wameonekana nchini, ambayo ndiyo dalili zake ni zile zilizotajwa awali.
Aina ya pili ya Dengu, alisema ni ile ya damu, ambayo alisema dalili zake huonekana kwa damu kwenye fizi na aina ya tatu ni ile Dengu ambayo mgonjwa hupoteza fahamu.

Wanakozaliana
Naibu Waziri alitaja maeneo wanakozaliana mbu wanaosababisha ugonjwa huo ni sehemu ambayo watu hudharau, kama kwenye makopo ya kuoteshea maua majumbani, masalia ya vyakula katika vyombo vya nyumbani, kwenye makopo, katika mabaki ya vifuu vya nazi na kwenye matairi ya magari yaliyotelekezwa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger