MSANII mkongwe kunako gemu la filamu
Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kuwa hawezi kuachika kwenye ndoa
yake iliyodumu kwa miaka 13 na wanaosubiri aachwe, watasubiri sana.
Akizungumza na paparazi wetu juzi Cathy
alisema kuwa, amekuwa akizushiwa kwamba anatoka nje ya ndoa na wasanii
tofauti lakini hayo ni maneno tu ambayo hayamuumizi mumewe kwani ni
muelewa na hawezi kuyasikiliza.
“Ndoa yetu ina miaka 13 sasa,
nawashangaa sana wanaosema mimi nachepuka kwa kutoka na Dude,
ninachoweza kusema ni kwamba hata wakimwambia mume wangu hawezi kuniacha
maana mimi na yeye tulianzia mbali sana, kusikiliza umbeya wa watu ni
kupoteza muda,” alisema Cathy.
0 comments:
Post a Comment