STAA wa filamu za Kibongo, Aisha Bui
amepata mtoto wa kike aliyejifungua kwa njia ya upasuaji lakini kumekuwa
na usiri mkubwa katika jambo hilo.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Aisha alisema anamshukuru Mungu kwa kumjaalia mtoto wa kike aliyempa jina la Saloma.
“Nimefurahi sana, kumpata mtoto ni jambo
la kumshukuru Mungu na sasa najisikia raha sana kuitwa mama,” alisema
Aisha na kuongeza kuwa, mwanaume aliyezaa naye ni mchumba wake wa siku
nyingi ambaye anaishi nje ya nchi na wanatarajia kufunga ndoa siku si
nyingi.
0 comments:
Post a Comment