STAA wa
filamu za Kibongo, Rose Ndauka amezidi kulilia ndoa ambapo sasa
ameonesha shauku ya kufunga hata ndoa ya mkeka ili kukata kiu yake
ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu.
Rose aliyejifungua hivi karibuni huku
baba wa mtoto akijulikana kwa jina moja la Malick alisema hayo hivi
karibuni nyumbani kwake Magomeni, Dar, ambako alikutana na mwandishi
wetu aliyetaka kujua ndoa ya msanii huyo itafungwa lini?
“Nimeshasubiri sana, nimejiandaa kwa
kila kitu hata upande wa dini niko tayari kwenda sambamba na mume wangu
mtarajiwa, naamini siku chache zijazo nitaolewa,” alisema Rose ambaye
uchumba wake umekuwa ukifunikwa na sintofahamu kibao.
Rose aliongeza kuwa siku atakayofunga ndoa furaha yake itakuwa mara dufu kwa sababu tayari ana ‘baby’
0 comments:
Post a Comment