Rada na matunguri yanayosadikiwa kuangushwa usiku na wachawi kutoka
angani vimezua tafrani la aina yake jirani na kanisa la kilokole, Risasi
Jumamosi lina mzigo kamili.
Mwinjilisti ambaye jina lake halikufahamika mara moja akikagua vifaa vya wachawi baada ya kuangushwa.
Tukio hilo la aina yake lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu maeneo ya
Tazara-Maghorofani, Dar hivyo kuibua hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo
wakihofia kulogwa.
Habari zilieleza kwamba alfajiri ya siku ya tukio hilo, watu waliona matunguri kwenye uchochoro unaokatiza katika nyumba zao.
Ilielezwa kwamba baadhi ya watu walidai kuwa matunguri hayo
yalidondoshwa na wachawi waliopita eneo hilo wakielekea kuwaloga watu
mahali fulani na kuongeza kuwa inawezekana kutokana na kanisa kuwa
karibu na eneo hilo ndipo wakapata tafrani angani kiasi cha kudondosha
rada zao.
“Hapa lazima wachawi walikuwa wanakwenda kuloga sehemu, lakini kutokana
na kanisa kuwa karibu na njia zao wakajikuta wakipita kwa tabu. Mwishowe
wakadondosha mizigo yao,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Ilidaiwa kuwa umati uliofurika eneo hilo ulipatwa na wasiwasi na
kutafuta msaada wa kiroho kwa kuwatafuta wachungaji wa kanisa hilo
ambapo walikutana na wainjilisti wawili ambao walifika eneo la tukio na
kuvikusanya vifaa hivyo kwenye kiroba huku wakiviombea.
Baadhi ya vifaa vilivyoshuhudiwa
na waandishi wetu ni vibuyu vilivyozungushiwa vitambaa vyekundu, shanga
zilizotengenezwa kwa makasha ya konokono wa baharini, vyupa
vilivyoonekana kuwa na dawa za mitishamba, kibuyu kikubwa chenye maji
meusi na pembe kubwa ambalo lilidaiwa ndiyo rada inayotumika kuongozea
ungo.
Kuhusu maji meusi ilidaiwa kuwa hutumiwa na wachawi wasionekane wakiwa katika shughuli zao.
Wakizungumza na waandishi wetu baada ya kuvikabidhi vifaa hivyo kanisani kwa ajili ya kuvichoma, wainjilisti hao waliojitambulisha kwa majina ya Amos Beda na Innocent Gervas wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) walisema kuwa, vifaa hivyo vinaonekana kuwa na uhusiano mkubwa na nguvu za giza.Walimtaka mwenye navyo kujitokeza kanisani ili amrudie Mungu.
Imeandaliwa na Chande Abdallah, Degratius Mongela na Denis Mtima

0 comments:
Post a Comment