Rei alikamatwa katika msako wa polisi katikati ya Jiji la Dar (City Center) hivi karibuni akiwa na kundi la warembo wa vyuo mbalimbali wakifanya biashara haramu ya kuuza miili.
Mrembo huyo ambaye Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilimshuhudia, kabla ya kupelekwa kituo kikuu cha polisi, Wilaya ya Ilala (Central), alijitetea kuwa yeye ni denti wa chuo kikuu hivyo kitendo cha kupigwa picha alijua kabisa kuwa zitasambaa mitandaoni hivyo itakuwa ni aibu kubwa.
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wakichukua picha. “Kaka naomba usinitoe gazetini au mitandaoni, haya ni maisha tu, itakuwa aibu kwa wanachuo wenzangu,” alijitetea. Mbali na hayo, mrembo huyo wa haja alikuwa akihaha kuwa kama ishu hiyo itamfikia mchungaji wake, basi hatakuwa na sehemu ya kuficha uso wake. Pia Rei alijitetea kuwa huwa hajiuzi kila siku na hiyo ilitokea tu kwa bahati mbaya kwani ana biashara zake binafsi.
0 comments:
Post a Comment