Friday, 20 June 2014

NEC: KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini, kulia ni Mkurugenzi wa uchaguzi toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Mallaba.
2_2c151.jpg
Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarijia kuanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mapema mwezi Septemba 2014, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na upikaji wa Kura za Maoni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva wakati akifungua Mkutano wa NEC na Wahariri wa Vyombo vya Habari, leo jijini Dar es Salaam.
Jaji Lubuva amebainisha kuwa uborehasji wa Daftari la Wapiga kura litatumia mfumo mpya wa Kiteknolojia ujulikanao kama Biometric Voter Registration (BVR) ambapo katika mfumo huo taarifa za mtu za Kibiolojia au tabia ya mwanadamu zitachukuliwa na kuifadhiwa kwenye kanzi data ya Wapiga Kura.
Katika mfumo huo wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na Kadi za Mpiga Kura watatakiwa kuandikishwa upya ili kupata Daftari sahihi linaloaminika zaidi kwa ajili ya upigaji Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Uamuzi wa kutumia mfumo huo mpya wa kuandikisha wapiga kura umefikiwa baada ya kubaini kasoro mbalimbali zilizokuwepo kutokana nma kutumia mfumo wa zamani wa Optical Mark Recognition (OMR) hadi kupelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kupigia kelele mfumo huo,
Aliongeza kuwa kutumiika kwa mfumo wa BRV kutasaidi kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja.
“Ndugu zangu wahariri ni ukweli ulio dhahiri kwamba matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa na kasoro,zilizopelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake. Hivyo ni mategemeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa matumizi ya BVR yatapunguza au kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo”. Alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kutoa ushirikiano kwa NEC ilikufanikisha zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura kwa kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi ili waapate uekewa wa mfumo huu mpya utakaomtumika katika zoezi hilo, na kutoa hamasa wajitokeze katika viotuo vya kujiandikishia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba amesema kuwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya uhakiki wa vituo vya kujiandikishia ambapo jumla ya vituo 40,015 vimeainishwa kutoka vituo 24,919 vilivyokuwepo awali.
Malaba aliongeza kuwa ongezeko hilo la vituo limetokana na kushusha zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kutoka ngazi ya Kata, na sasa utafanyika kuanzia ngazi ya Vitongoj,Vijijii na Mitaa ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.
Malaba aliongeza kuwa Tume inatarijia kupokea vifaa kwa ajili ya zoezi hilo mapema mwezi Aguosti 2014 kwa aijili ya  kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura, na kuongeza kuwa vifaa vichache vitawasili mapema mwezi julai kufanikisha mafunzo kwa watendaji watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linatarijiwa kuanza mwezi septemba 2014 ambapo kila kituo cha kujiandikisha kinakadiriwa kutumia siku 14 hadi zoezi kukamilika , na jumla ya takribani shilingi Bilioni 293 zinatarajiwa kutumika katika zoezi hilo
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger