ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Pangawe mkoani Morogoro wamemuokota mtoto mwenye umri wa miaka sita, Mwajuma Athuman aliyedai kukimbia mateso kutoka kwa mama yake mkubwa Juni 17, mwaka huu.
Mwajuma
Athuman akiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Mohamed Said,
aliyejifunika (kulia) ni mama anayedaiwa kumtesa mtoto huyo.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinasema Mwajuma ambaye ni
mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge mjini hapa, aliokotwa katika
vichaka vilivyopo pembeni ya kambi hiyo akitokea Kijiji cha Ngionolo
kilichopo jirani ambako ndiko anakoishi mama yake mkubwa aliyetajwa kwa
jina moja la Ashura ambaye ni mganga wa kienyeji.
Baada ya kumuokota na kumhoji, wanajeshi hao walimpeleka kwa mjumbe,
Magessa Mwita ambaye naye alimpeleka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
wa Tangi la Maji, Mohamed Said.Mwandishi wa habari hizi alimkuta mtoto huyo akiwa na makovu kichwani na kidonda kikubwa mguuni kilichosababisha ashindwe kutembea ambapo alidai kilitokana na kipigo kutoka kwa mama yake huyo.
“Nimekimbia nyumbani, mama ananipiga kila siku nikitoka shuleni, nilifika kambi ya jeshi kwa mtoto mwenzangu ninayesoma naye lakini nilipotea nyumba yao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mohamed Said akiwa na huzuni kutokana na tukio hilo.
“Nilipoona giza linaingia nikaamua kutafuta kichaka nilale ili
asubuhi niende shule halafu niondoke na rafiki yangu nikaishi kwao. Juzi
ndiyo askari walinikuta na kunileta hapa,” alisema mtoto huyo.Kuhusu wazazi wake, mtoto huyo alisema mama yake alifariki dunia yeye akiwa na umri wa miaka miwili, baba yake anaishi Mwanza ambako ameoa mke mwingine. Mama mkubwa huyo huyo alipoitwa mbele ya viongozi wa serikali ya mitaa, alikiri kuishi na mtoto huyo, lakini alikanusha kumtesa.
Hata hivyo, mwanamke huyo alingĂangĂania kumchukua mtoto wake ili arejee naye nyumbani, lakini viongozi hao waligoma na kwa zaidi ya siku nne aliishi nyumbani kwa Mohamed Said.
Katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa serikali ya mtaa na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, mama mkubwa huyo na mwandishi wa habari hizi walikubaliana kuwasiliana na mjomba wa mtoto aishiye jijini Dar, Anjelu Shindano ambaye aliahidi kutuma nauli ili mtoto huyo aweze kwenda Mwanza kwa baba yake.
0 comments:
Post a Comment