MAJANGA! Siku
chache baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka
shemejiye, mwimbaji wa Injili na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha
amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na viwanja.
Chanzo makini kilichomo ndani ya
familia, kimedai kuwa mara baada ya Mbasha kujitokeza na kuwekwa
mahabusu Juni 17, mwaka huu, mtu asiyejulikana alikwenda nyumbani kwa
mfanyabiashara huyo, Tabata-Kimanga, Dar na kukwapua hati za nyumba na
viwanja mbalimbali anavyovimiliki.
...Siku aliyopandishwa kizimbani.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani,
vilikombwa vyote sijui na nani. Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza
ametoka mahabusu halafu anakuta nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama
hivyo, inasikitisha sana,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo hicho
kilisema katika vitu vilivyoibwa ni pamoja na nyaraka mbalimbali
zikiwemo hati za viwanja kadhaa vilivyopo Iringa, kadi ya gari na vitu
vingine vidogovidogo.
Baada ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ili kujua ukweli wa ishu hiyo ambapo alipopatikana alikiri kutovikuta vitu hivyo muhimu nyumbani kwake.
“Ni kweli kama ulivyosikia ila nisingependa kuzungumzia kila kitu kwa sasa nahitaji kupumzisha akili,” alisema Mbasha.

Mbasha aliyetoka kwa dhamana Juni 19,
katika kesi hiyo ya kudaiwa kubaka iliyosomwa katika Mahakama ya Wilaya
ya Ilala, kesi yake itatajwa tena Julai 17, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment