Ahmed Musa (kulia) akishangilia na wenzake wa Nigeria baada ya kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Argentina.
KIKOSI cha Nigeria kimefanikiwa kuingia
hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 inayoendelea nchini
Brazil usiku huu.
Nigeria wametinga hatua hiyo wakiwa na pointi 4 mbali na kupoteza mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwa mabao 3-2. Wamefuzu katika kundi F wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Argentina.
Timu nyingine za Afrika ambazo bado zinategemewa na mashabiki ni Algeria kutoka kundi H na Ghana ya kundi G. Timu za Afrika zilizoaga mashindano hayo mpaka sasa ni Cameroon na Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment