Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta
utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na
vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya
uandishi wa habari.
Hayo
yalisemwa na mkurugenzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa
mamlaka hiyo, Dk Joseph Kilongola katika kongamano la kimataifa la
habari lililo andaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na
kufanyika jijini hapa kwa mara ya kwanza, mwaka huu.
“Licha
ya kuwaelimisha wadau wa habari hasa wamiliki wa ‘blog’ juu ya
kuzingatia maadili ya uandishi kwa kila wapakiacho mtandaoni, sasa
tunakuja na cyber security itakayosimamia upashanaji habari,” alisema Dk Kilongola.
Alisema
mfumo huo utafanya pia kazi ya kuchuja habari zote kabla hazijawekwa
mtandaoni na utatoa ulinzi kwa jambo lolote linalotishia usalama katika
sekta yoyote ya uchumi na kabla madhara hayajatokea, wahusika watakuwa
wameshajulikana.
Profesa
Florens Luoga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
alitahadharisha dhidi uhuru na haki ya matumizi ya majukwaa mbalimbali
ya mawasiliano kuwa yanapaswa kuzingatia maadili ili kuepusha athari
zinazoweza kujitokea katika jamii.
“Kila
teknolojia mpya huja na athari zake. Maendeleo ya teknolojia ya habari
nayo yamekumbwa na hilo. Athari zake zimeanza kujitokeza.
“Maadili
ya kitaaluma ni vyema yakazingatiwa na wote wanaojihusisha na
upashanaji habari ili kuchangia maendeleo yaliyokusudiwa,” alisema Profesa Luoga.
Alihimiza wataalamu wa habari kuhudhuria makongamano ya kitaaluma yanayoandaliwa.
0 comments:
Post a Comment