Monday, 30 June 2014

CCM YAWABEMBELEZA CUF KUREJEA BUNGE LA KATIBA-MWEZI WA NANE

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,Vuai Ali Vuai
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ali Vuai, amesema ikiwa wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba kutoka Chama cha Wananchi (CUF) hawatorejea bungeni, wataikosesha Zanzibar fursa za kiuchumi.

Alisema ni vyema wajumbe hao kurejea bungeni na kushirikiana na CCM kuitetea Zanzibar kupata fursa za kiuchumi kwa maslahi ya Wazanzibari.
“Nawambia CUF wasisusie Bunge la Katiba, nawaomba warudi bungeni ili tukae pamoja na kuitetea Zanzibar kupata fursa za kiuchumi ikiwamo masuala ya mafuta,” alisema Vuai juzi jioni wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM na kufanyika katika Jimbo la Mjimkongwe.
Vuai alisema kuwa ili masuala ya mafuta yawe mali ya Zanzibar, ni lazima CUF na CCM kukaa pamoja na kulijadili suala hilo katika Bunge la Katiba ili katiba itakayoundwa iweze kutoa fursa mafuta yasiwamo katika orodha ya mambo ya Muungano.
Alisema wakati umefika sasa kuondoa itikadi za kisiasa na kujadili mambo ya msingi ambayo yataweza kuleta maendeleo kwa Wazanzibari. “Endapo CUF hawatarudi katika Bunge la Katiba Zanzibar itaathirika kiuchumi,
tusidanganyane hakuna njia ya mkato ya kuweza kuyatoa masuala ya mafuta katika Muungano bila ya kukaa pamoja na kujadiliana,” alisema Vuai.
Aliwataka viongozi wa CUF kufahamu kuwa marekebisho ya katiba sura ya sita yaliofanywa na CCM katika bunge hilo yanamanufaa kwa Zanzibar hivyo wanapaswa kuyaunga mkono.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger