Mwanamke
mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Asha (31) ambaye ni mke wa mtu,
amejikuta akiachika katika ndoa yake baada ya kudaiwa kumuunguza midomo
mwanaye, huko Yombo Buza, jijini Dar, Juni 24 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa majirani, mwanamke huyo alimchoma mtoto wake wa kumzaa,
Paulina, mwenye umri wa miaka mitano kwa kile alichodai kuwa tabia yake
ya kudokoadokoa fedha za mtaji wake wa biashara ya samaki.
Majirani
hao walisema kuwa walimuona mama huyo akichochea moto wa kuni katika
jiko lililokuwa nje ya nyumba yake, kabla ya kuingia ndani akiwa na fito
moja inayowaka na muda mfupi baadaye wakasikia mtoto huyo akilia kwa
sauti iliyoonyesha kupata maumivu makali.
Kilio
hicho kiliwashtua majirani hao ambao waliamua kuingia ndani ya nyumba
hiyo, lakini katika hali ya kushangaza, walimkuta mama huyo ameshikilia
kuni yenye moto huku mtoto huyo akiwa na majeraha ya kuchomwa moto
midomoni na mguuni.
Baada
ya kuona hivyo, walimshurutisha kuacha unyama huo na badala yake
ampeleke hospitali, lakini mama huyo alikataa katakata, akidai hawezi
kufanya hivyo hadi binti huyo mdogo atakapoacha tabia yake.
Kuona hivyo, majirani hao walitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Buza ambapo askari walifika eneo la tukio wakiongozana na mwanaharakati wa haki za watoto kutoka taasisi binafsi ya Tuhimizane Children Academy, Cleophas Simeone, ambao walimkamata na kumfikisha kituoni alikofunguliwa jalada lenye namba CHA/RB/5521/2014, UKATILI DHIDI YA MTOTO.
Mwanaharakati
huyo aliwasiliana kwa njia ya simu na baba mzazi wa mtoto huyo aliyedai
yupo nje ya Dar es Salaam kikazi ambapo baada ya kusimuliwa
kilichotokea, aliagiza mwanamke huyo kuondoka nyumbani kwake muda huohuo
na kumuomba Simeone aendelee kukaa na mwanaye ambaye ameshaanza
matibabu, hadi atakaporejea
0 comments:
Post a Comment