Sunday, 22 June 2014

JAHAZI MODERN TAARAB: YAZINDUA ALBAMU MPYA IITWAYO 'CHOZI LA MAMA'

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Meneja wa Jahazi Modern Taarab, Mohammed Rashid Mauji 'Father Mauji' pamoja na shabiki wa Jahazi wakizindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama
.
Mzee Yusuf akisema na mashabiki wake wakati wa uzinduzi huo.
Mwimbaji nyota wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuf (kulia) akiongea jambo kabla ya uzinduzi wa Chozi la Mama. Katikati ni Aisha Abushily 'Mama wa madikodiko' kutoka Pilipili FM ya Kenya.
Mzee Yusuf akiimba wimbo wa Chozi la Mama uliobeba jina la albamu iliyozinduliwa usiku huu Dar Live.
Mashabiki wa Jahazi wakifuatilia uzinduzi huo muda huu.
Albamu mpya ya Chozi la Mama iliyozinduliwa usiku huu.
Madansa wa Mzee Yusuf wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akicharaza kinanda kwa mbwembwe.
...Mashabiki wakimtunza Mzee Yusuf.
Khadija Yusuf akitoa burudani ndani ya Dar Live wakati wa uzinduzi wa Chozi la Mama.
MC wa leo katika uzinduzi wa albamu mpya ya Jahazi, Aisha Abushily 'Mama  wa madikodiko' (kushoto)  akiwa katika pozi na Leila Salim 'Aunt Liloo' wote  kutoka Mombasa, Kenya.
Wadau wa Jahazi, Injinia Arnold Gabone (kushoto) na mwenzake wakiwa katika pozi wakati wa uzinduzi wa Chozi la Mama.
Mzee Yusuf akihojiwa na Global TV Online baada ya uzunduzi.
Burudani zikiwa zimepamba moto Dar Live.
Jahazi Modern Taarab chini ya kiongozi wake Mzee Yusuf 'Mfalme' imezindua albamu mpya iitwayo Chozi la Mama yenye jumla ya nyimbo sita usiku huu ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakheem jijini Dar. Albamu hiyo ni ya 10 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger