Katika hali ya kushangaza, mwanamke
mmoja aliyefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli hivi karibuni aliamua
kukabidhi kanisani shanga za majini kwa kile alichodai kuwa, zimekuwa
zikimtesa na kumfanya akose amani.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani hapa baada ya moto wa
Injili kuwashwa na Mchungaji Kiongozi, Frank Endrew.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa
waumini wanaosali kanisani hapo aliyejitambulisha kwa jina la Yusta
John alisema, awali mwanamke huyo alionekana mwenye jambo linalomtatiza
na lilipotolewa tangazo la wenye matatizo kupita mbele, Asnath alifanya
hivyo huku akiwa ameshika shanga mkononi.
“Watu wengi walikuwa na shauku ya kujua
lililomsibu mama huyo lakini alipofika alimkabidhi mchungaji Frank
shanga hizo zilizotengenezwa kiasili zinazodaiwa ni za majini.
“Mwenyewe alieleza kuwa, alipewa kama zawadi na mwanaye lakini cha ajabu zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
0 comments:
Post a Comment