Kwa taarifa tulizozipata hivi punde ni kwamba ‘wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) wanajiandaa kuandamana kushinikiza kupewa hela zao za mafunzo kwa vitendo’ mtoa taarifa amesema chuo ilishapokea pesa hizo tangu wiki mbili zilizopita lakini mpaka sasa bado wanafunzi hawapewa KUSAINI pesa hizo. Na ukisoma
magazeti ya leo tar 27th June 2014, moja ya gazeti limeandika “UDOM inarudisha pesa za mafunzo kwa vitendo Bodi ya mikopo(HSLB), gazeti limemunukuu mmoja wa viogozi wakuu wa UDOM, Kwa maana hiyo kuwa ni kweli pesa ipo lakini WATAWALA hawataki kuitoa, Mimi na wewe hatujui ila lazima tujiulize maswali kazaaa 1) 1) Kwanini kila siku UDOM…? ikumbukwe kuwa tar 16th june palikuwa na mgomo wa WAHAZIRI wa chuo hichohicho waliokuwa wakishinikza kulipwa hela zao za kusimamia mitihani, mwezi wa 5mwaka huu palikuwa na mgomo pia wa wanafunzi kushinikiza kulipwa pesa zao za CHAKULA na MALAZI. 2) 2) Je? Mkataba wa mkopo ni kati Bodi ya mikopo(HESLB) na mwanafunzi? AMA chuo na mwanafunzi? Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa “Mwanafunzi ndiye aliyeingia mkataba na Bodi(HESLB) na chuo ni kama daraja tu (intermediary) wa kufikisha pesa kwa wanafunzi, swali la kujiuliza kwanini UDOM wamepewa hela za wanafunzi halafu wanataka kurudisha..? 3) 3) Kama wanafunzi walianza kumaliza mitihan yao J3 na wengine wanamalizia leo, je hao waliomaliza J3 wanafanya nini mpaka sasa? Sasa isifike wakati watoto wetu waanze kujiunza kwa sababu ya kuzuiliwa pesa yao halali waliyoingia mkataba na bodi na siyo chuo. Sina mengi kwa sasa tutakuwa tunapeana taarifa kwa kinachoendelea (up date ya kinachojiri), maana nimepewa News kuwa saa 11:45 jion hii kuna kikao kikubwa UDOM…
0 comments:
Post a Comment