Wapiganaji wa kisunni wamekuwa wakiteka miji nchini Iraq na kuwaacha maelfu bila makao
Wapiganaji
wa Kisunni nchini Iraq wameteka kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha
mafuta nchini humo katika eneo la Baiji Kaskazini mwa Baghdad.
Kiwanda hicho kilikuwa kimezingirwa kwa kipindi cha siku kumi huku vikosi vya serikali vikizuia shambulizi la waasi mara kadhaa.
Msemaji
wawaasi hao amesema kuwa kiwanda hicho sasa kitapewa usimamizi wa
makabila yanayoishi katika eneo hilo na kwamba mapambano ya kuuteka mji
mkuu wa Baghdad yataendelea.
Utekaji
nyara wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Baiji ni muhimu sana kwa waasi
hao iwapo watasimamia maeneo ambayo wameyateka kufikia sasa, hasa kwa
kutoa umeme kwa mji wa Mosul.
Wakati
huo huo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, ameahidi
msaada mkubwa kwa jeshi la Iraq wakati wapiganaji wa Kisunni wakiendelea
na mashambulizi yao nchini humo.
Alisema
Waziri Mkuu, Nouri al-Maliki na viongozi wengine wameahidi kuunda
Serikali ya Umoja inayowashirikisha wote ifikapo mwisho wa mwezi.
Kiwanda cha mafuta ambacho kimedhibitiwa na waasi wa kisunni
Daktari
Zuhair Al-Naher, msemaji wa Serikali ya Iraq ambaye pia ni mwanachama wa
chama tawala cha Waziri Mkuu Nouri al-Maliki, Islamic Dawa Party,
anasema kuwa anaamini kuwa Bwana Maliki ataunda Serikali ya
kuwashirikisha wote.
Bwana Kerry alikuja Baghdad kwa mambo mawili.
Kwanza
kabisa kumshinikiza Waziri Mkuu Nouri al-Maliki na viongozi wengine wa
kisiasa kuwa wanapaswa kuwa na Serikali mpya, pana inayofuatia uchaguzi
mkuu uliofanywa Aprili. Mamlaka yanapaswa kugawiwa Wasunni na Wakurdi
walio wachache na sio kwa Washia ambao ni wengi pekee.
Pili
Bwana Kerry alitaka kuhakikishia Serikali ya Iraq kuwa Marekani
itasaidia wanajeshi wa taifa hilo wanapendelea kupambana na wapiganaji
wa Kiislamu wa kundi la ISIS.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment