Tukio hilo la aina yake lilijiri Juni
wikiendi iliyopita maeneo ya Somanga-Magomeni, Dar ambapo kwa mujibu wa
wasamaria wema waliomuona mtoto huyo, alionekana majira ya asubuhi
akirandaranda barabarani.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Walisema walidhani alikuwa akielekea nyumbani kwao lakini hadi jioni walishangaa kumuona bado anarandaranda mitaani mwenyewe.
Mtoto huyo akiwa na msamaria.
Baadaye OFM ilipewa taarifa na kufika
eneo la tukio ambapo ilipata maelezo kuwa mama wa mtoto huyo huwa na
tabia ya kumwacha mwanaye mara kwa mara mtaani bila kumjali.
OFM ilifikisha suala hilo kwa mjumbe wa mtaa huo ambaye alimtambua mtoto huyo mara moja kwa kuwa alikuwa akiishi naye nyumba moja hivyo alimpeleka kwa wazazi wake huku akiwapa onyo kali.
0 comments:
Post a Comment