Friday, 27 June 2014

MZEE WA KANISA AKURUPUSHWA GESTI-BAADA YA KUFUMANIWA NA BINTI WA KIZAI KIPYA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Tumekwisha! Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora Jacob, Ijumaa lina kisanga cha aina yake.

Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.
Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.
OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.
Akiwa kwenye geti la kanisa.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!
Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.
OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.
.....akitaitiwa.
Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.
ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.
APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Mtuhumiwa akitembezwa mtaani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger