Mauaji
hayo ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo,baada ya
majambazi hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi
huyo na familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia
kwa bapa za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika
kuwapa kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka katika
taasisi moja ya fedha.
Afisa
upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati
Mlashan,akizungumza na ITV akiwa eneo la tukio, amesema baada ya
majambazi hayo kuvunja milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi
tatu na moja kumpata kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia
papo hapo na kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo
ili kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi serikali katika kata ya
Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao
baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM,wameliomba
jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao utawesha kukamatwa kwa
wahusika,hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa
waliyonayo sasa.
0 comments:
Post a Comment