“Eeh Mungu sikia kilio changu unisaidie!” Ndivyo alivyoanza kusimulia mtoto Salum Kassim (16), mkazi wa Kilimahewa-Tandika, Dar, ambaye ameteseka kwa muda wa miaka minne (siku 1440) akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Akizungumza kwa maumivu makali na wanahabari wetu nyumbani kwao maeneo hayo, Salum alisema tatizo hilo la moyo limemsababishia matatizo mengine ya kiafya kama moyo kujaa maji, kuvimba tumbo, kushindwa kuhema, kukaa vizuri, kulala na kutembea.
Salum alisimulia kuwa mateso anayoyapata
kupitia ugonjwa huo yamemfanya kushindwa kuendelea na masomo kwani
aliacha akiwa darasa la tano katika Shule ya Msingi ya Moma iliyopo
mkoani Mtwara, hivyo kuanza kuhangaika na matibabu hadi mwaka 2012
alipohamishiwa Hospitali ya Muhimbili, Dar kwa matibabu zaidi.Muonekano wa uvimbe wa tumbo aliokuwa nao Salum Kassim.
Alisema kuwa baada ya kufika Dar na kuanza matibabu, amejikuta
akikabiliwa na changamoto nyingi kwani kila kitu kwake ni shida kutokana
na ugumu wa maisha na kushindwa kupata matibabu ya ugonjwa wake achilia
mbali chakula na malazi.Alieleza kuwa kuna wakati anakosa dawa kutokana na baba yake ambaye anaishi naye kukosa fedha ya kununulia dawa na zaidi amekuwa akipata msaada kutoka kwa mama wa jirani.
Alisema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuna baadhi ya vyakula alivyokatazwa lakini anakula kwa sababu ya ugumu wa maisha.
“Mara nyingine tunashindwa kwenda kufuata dawa kwa sababu baba mdogo anakuwa hana fedha.
“Ikitokea hivyo huwa ninakaa bila kuendelea na dozi hadi anapopata ndiyo naendelea,” alisema kwa uchungu.
Salum aliomba Watanzania wamsaidie ili apate matibabu na kurejea katika hali yake ya kawaida na kuendelea na masomo.
“Watanzania naombeni sana msaada wa hali na mali ili nipate matibabu ya huu ugonjwa kwani nimeteseka kwa kipindi kirefu.
“Ukweli sijui hatima yangu. Eeh Mungu nisaidie,” alisema.
Kaka wa Salum aliyejitambulisha kwa jina la Issa Kassim aliwaomba wasamaria wema kumsaidia mdogo wake kwa kwa hali na mali ili kunusuru uhai wake.
Kwa yeyote anayeguswa moyoni mwake na anaweza kumsaidia mtoto Salum, awasiliane naye kupitia simu namba 0785999276 na 0682865248 ambazo ni za baba mdogo wa Salum aitwaye Kassim au fika katika ofisi zetu za Global Publishers, Bamaga-Mwenge,
Dar. Kutoa ni moyo si utajiri.
0 comments:
Post a Comment