Thursday, 26 June 2014

MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA JANA MKOANI GEITA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY







KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA  KAMISHINA MSAIDIZI JOSEPH KONYO AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG  ILIYOKUWA INATUMIWA NA MAJAMBAZI JANA

Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita.

 Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.

Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi ambacho hakijafahamika na   kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger