Licha ya
kukabiliwa na marufuku ya FIFA ya miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa
Italia Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya
kumsajili mshambulizi machachari wa wa Uruguay Luiz Suarez.
Mshambulizi
huyo wa kutegemewa wa klabu ya Liverpool ya Uingereza amepigwa marufuku
ya miezi minne kumaanisha kuwa hatoshiriki mechi yeyote hadi mwezi
Oktoba.
Aidha Suarez hatoweza hata kufanya mazoezi katika kipindi hicho.
Haijulikani
kwanini mabingwa hao wa zamani wa kombe la mabingwa barani uropa ambao
wanajivunia huduma za Lionel Messi wa Argentina na Neymarwa Brazil bado
wanamtaka Suarez.
Liverpool ilimnunua Suarez kwa pauni milioni £25m mwezi Januari 2011 kutoka klabu ya Ajax.
Hii si
mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama
hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa
mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea
Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia
Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota
huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani
kutoka Brazil.
0 comments:
Post a Comment