Kufuatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo, mwigizaji Baby Joseph Madaha amelazimika kubadili mtindo wake wa maisha na kuishi kitakatifu.
Staa wa filamu Bongo Baby Joseph Madaha
Akipiga stori na paparazi wetu, Baby Madaha alisema anawasihi hata
wasanii wenzake wabadili mfumo wa maisha kwa kumgeukia Mungu na kufanya
ibada kila mara kwa kuwa vifo hivyo vinawapa somo la kuwakumbusha
kumkaribia Mungu.“Nimebadili mfumo wa maisha kwa kufanya ibada na ninawashauri wasanii wenzangu tumgeukie Mungu kwani vifo na mambo yanayotokea yanatukumbusha ibada na kujiweka safi,” alisema Baby Madaha.
0 comments:
Post a Comment