Brass Band wakitoa heshima kwa ala za muziki.
Kamishna wa Magereza kutoka Namibia, Raphael Hamunyela akipanda mti eneo la Gereza la Ukonga.
ASKARI magereza jana walisherekea siku ya
magereza katika chuo cha Ukonga Dar. Maadhimisho hayo yalisindikiza na
burudani mbalimbali ikiwemo gwaride la askari, michezo ya judo na
muziki.
Lengo la maadhimisho hayo ni kuielimsha
jamii kuwa gerezani si eneo la mateso bali kujirekebisha na kujifunza
mambo mbalimbali ikiwemo ufundi, kilimo, ufugaji na fani nyinginezo .
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa
ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Mathias Chikawe ambapo katika hutuba
yake aliahidi kupeleka ombi la msamaha wa wafungwa kwa Rais Jakaya
Kikwete kama walivyoomba wafungwa.
0 comments:
Post a Comment