Tuesday, 24 June 2014

KANGA MOJA:HUYU HAPA YULE MAMA ALIEPIGWA RISASI WAKATI WAKISHIRIKI NGOMA HIZO

...
MAMA mzazi wa binti aliyesababisha wasichana wawili kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kushiriki ngoma maarufu ya Kanga Moko iliyopigwa marufuku, huko Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam, amefunguka na kusema kuwa hakukuwa na sherehe yoyote nyumbani kwake siku hiyo ya tukio.
Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, aliyepigwa risasi katika paja la kulia wakati wa vurugu iliyotokea.
Mama huyo, Rehema Aziz alisema waliojeruhiwa walikuwa wakisherehekea kuolewa kwa mwanaye aitwaye Aziza Aziz, ambao walikuwa ni marafiki zake na walifanya hivyo kwa mujibu wa mila za watu wa Pwani, za kucheza na kufurahi wakizunguka mitaani, lakini bila kufanya fujo yoyote.

“Huo ulikuwa ni Mdundiko wa kawaida, tokea zamani tulikuwa hatuombi kibali na wao walifanya hivyo kama mila zinavyosema, siku ya tukio Juni 18, mwaka huu hatukuwa na sherehe hapa nyumbani isipokuwa jana yake ndiyo kulikuwa na sherehe ya kumpa zawadi mwanangu.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis (20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio.
“Tukio la Juni 18, wasichana ambao ni marafiki zake mwanangu ambaye kwa sasa yupo kwa mume wake, walikuwa wakisherehekea wenyewe kivyao, bila mimi kujua, lakini hata hivyo mbona ilikuwa ni mapema mno, saa kumi jioni na walikuwa ni wanawake tu,” alisema mama huyo.
Kwa upande wake majeruhi Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, alisema anachokijua ni kwa alipigwa risasi katika paja la kulia wakati huo wa vurugu ya kuwataka watawanyike.
“Sisi tulikuwa tukiwasindikiza watu wa tarumbeta ambao walikuwa wanaume, tuliobaki tulikuwa wanawake na hakukuwa na vurugu wala hatukumpiga askari ila sisi tumepigwa risasi kama swala,” alisema Grace.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis (20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio, alisema ameshangazwa na kitendo hicho.
Walisema ni jambo la ajabu kuwa polisi walitumia nguvu kubwa dhidi ya wanawake waliokuwa hawana silaha yoyote.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Husna Nondo alisema watu hao hawakuwa na kibali cha aina yoyote na kusisitiza kuwa serikali imeshapiga marufuku ngoma za Kanga Moko hivyo amewataka wananchi kufuata agizo hilo la serikali.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema upelelezi unaendelea ili kubaini tatizo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger