Kanali
Ally Hassan Mwanakatwe alizaliwa
tarehe 05 Julai, 1949 katika Kijiji
cha Dareda, Kata ya Dareda, Tarafa ya Dareda, Wilaya ya Babati katika
Mkoa wa
Manyara. Alisoma Shule ya
Msingi Singe Wilaya ya Mbulu aliyohitimu kuanzia mwaka 1954 hadi mwaka 1962 na
baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari Kigonsera akiwa Mtahiniwa Binafsi
kuanzia mwaka 1969 hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka 1972. Alijiunga na
Jeshi la Kujenga Taifa tarehe 14 Septemba, 1964 kwa kujitolea kwa muda wa miaka
mitatu (3). Alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01
Julai, 1967 na kutunukiwa Kamisheni katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania tarehe 01 Julai, 1975. Marehemu alistaafu utumishi Jeshini tarehe 04 Julai, 2006 akiwa amelitumikia Jeshi
kwa muda wa miaka 39 na siku 4.
Katika
utumishi wake Jeshini, Marehemu Kanali Ally Hassan
Mwanakatwealihudhuria kozi mbalimbali ikiwemo kozi ya Afisa Mwanafunzi,
Tanzania, 1975, Kozi ya Organization, Israel, 1967, Stashahada ya
Uhasibu, Tanzania, 1968, Kozi ya Kamanda Patuni, Tanzania, 1977, kozi ya
Kamanda Kombania,Tanzania, 1982, Shahada ya Kwanza ya Sanaa, Tanzania,
1982, Masters of Arts in Public Administration, Tanzania, 1985, Kozi ya
Ukamanda na Unadhimu Canada 1988, Kozi ya Uangalizi wa Amani Tanzania,
1994.
Marehemu
Kanali Ally Hassan Mwanakatwe wakati wa utumishi wake Jeshini alishika
madaraka mbalimbali ikiwemo Mkufunzi,
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, 1969 – 71, Afisa Mnadhimu Makao Makuu
ya Jeshi la Kujenga Taifa, 1977 – 78, Kamanda
Kombania, Vita vya Kagera, 1978 – 79, Msaidizi wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
1983 – 84, Muhadhiri Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, 1984 – 87, Mkufunzi Mkuu Msaidizi Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi cha Maafisa, 1988 – 91, Afisa Mnadhimu, Makao Makuu ya
Jeshi, 1991 – 92, Mkufunzi High
Commanders Training Wing, 1992 – 95, Katibu Mkuu, Chama cha Mpira Tanzania
(FAT), 1993 – 97, Mkurugenzi wa Elimu, Makao Makuu ya Jeshi,
1998 – 2001, Afisa Mnadhimu, Baraza la Usalama la Taifa, 2001 – 04, Mkurugenzi
wa Makumbusho, Makao Makuu ya Jeshi, 2004 hadi alipostaafu utumishi Jeshini
tarehe 04 Julai, 2006.
Kwa
kutambua na kuthamini mchango wake katika kulitumikia Jeshi na kulinda Taifa,
Rais na Amiri Jeshi Mkuu alimtunuku medali mbalimbali zikiwemo medali ya Vita
vya Kagera, Miaka 20 ya JWTZ, Miaka 40 ya JWTZ, Utumishi Mrefu Tanzania, na Utumishi Uliotukuka Tanzania.
Marehemu Kanali Ally Hassan Mwanakatwe alifariki dunia tarehe 07 Juni, 2014 katika Hospitali
ya Jeshi Lugalo alikopelekwa kwa matibabu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amin.
Askari wa Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Kanali (Mstaafu) Ally Hassan Mwanakatwe
katika hospitali kuu ya Jeshi, lugalo Dar es Salaam.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Kanali (mstaafu) Ally Hassan
Mwanakatwe katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
0 comments:
Post a Comment