“Mwenye
nyumba alibaki anasubiri alipwe kodi kwa kuwa alijua Geofrey aliingia
chumbani kwake kwa ajili ya kuchukua hela hiyo lakini muda mrefu ulipita
bila kutoka nje kiasi cha mwenye nyumba kuanza kupata wasiwasi lakini
aliamua kumuacha na kuondoka,” alisema ndugu huyo.
Ndugu
huyo alizidi kueleza kuwa, baada ya muda rafiki wa marehemu aitwaye
Dickson aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja ndiye aliyegundua mwenzake
alikuwa amejinyonga.
“Rafiki
yake aligonga sana mlango bila mafanikio ndipo alikwenda dirishani na
kuendelea kuita bila mafanikio, lakini alipochungulia alimuona Geofrey
akiwa ananing’inia ndipo alipotutaarifu tukaja,” alisema ndugu huyo.
Ndugu
huyo alisema baada ya taratibu za kipolisi kukamilika, walimsafirisha
marehemu mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi huku ikielezwa baba mwenye
nyumba na wanakamati wa harusi waliompa tenda marehemu wamesamehe madeni
yao.
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
0 comments:
Post a Comment