Muangalizi:
Jose Mourinho (kulia) amekuwa akiwatembelea watoto wanaosumbuliwa na
njaa pamoja na wagongwa wa UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi
wa Mpango wa Chakula Duniani.
BOSI
wa Chelsea, Jose Mourinho anadhani chama cha soka nchini England, FA
kingetoa faini za mpira wa miguu anazolipa kwa kuwasaida watu wenye
shida kama sehemu ya upendo.
Badala
ya kuangalia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil, Mourinho
amewatembelea watoto wanaosumbuliwa na njaa na wagonjwa wenye virusi vya
UKIMWI nchini Ivory Coast akiwa kama balozi wa umoja wa mataifa wa
Mpango wa Chakula Dunia.
Mreno
huyo alisema anataka kuona mpira unafanya kazi zaidi kusaidia mpango wa
Chakula Duniani (WFP) na akapendekeza FA itumie faini anazotozwa
kuwasaidia watu wenye shida.
"Nitalipa (faini) kwa tabasamu kama hela zinakwenda sehemu sahihi," Aliwaambia ITV wakati wa ziara yake.
'Huo
ni uzoefu, kwakweli nimepata uzoefu,". Alisema kocha huyo mwenye miaka
51 huku akishindwa kuzuia machozi yaliyokuwa yanamlenga.
"Na aina ya uzoefu ambapo najisikia kidogo".
"Ni machungu, lakini wakati fulani huwa ni nzuri kwa roho".
Mpango wa Chakula Dunia ni shirika kubwa la kimataifa linaloshughulikia balaa la njaa duniani kote.
Mwezi
mei, Mourinho alitozwa faini na FA ya Euro 10,000 kwa maneno yake
aliyosema juu ya viongozi wa mechi baada ya Chelsea kufungwa mabao 2-1
na Sunderland na kujikuta akivunja rekodi ya kucheza mechi 77 bila
kufungwa nyumbani.
Mourinho baada ya kutembelea Afrika amesisitiza faini zinazotozwa ligi kuu zipelekwa kusaidia wenye shida.
0 comments:
Post a Comment