Jeshi
la polisi mkoa wa Mara linamshikilia kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi
wa kidato cha 2 katika shule ya sekondari ya Kemoramba wilayani Butiama,
baada ya kutuhumiwa kumbaka mtoto wa kaka yeke mwenye umri wa mwaka
mmoja na miezi kumi, mkazi wa kijiji cha Nyankanga wilayani Butiama.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara ACP Paul Kasabago, amesema kuwa
mtoto huyo alibakwa hadi kuvunjwa mguu wake wa kushoto.
Mama
mzazi wa mtoto huyo Bi. Annaberi Waitara, akizungumzia tukio hilo akiwa
Hopitali ya Serikali Mkoa wa Mara Musoma, amesema kuwa mtoto wake
alibakwa na Shemeji yake huyo baada ya kumuachia wakati alipokwenda
kuchota maji kisimani
0 comments:
Post a Comment