Mume
aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar,
amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack
wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.Tukio
hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa
Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake
wakipeana maraha.
Imedaiwa
kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda katika
shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki yake na
kufanya mchezo wa kikubwa.
“Hata sisi wanawake tunaoishi
nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia lakini kinachotusikitisha
mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe ambaye anakuwa amekwenda
kazini,” alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani
mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo kwenda
kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za
kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni,
Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia ‘mchezo’
ukiendelea chumbani.
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa
kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki yake
lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni 1.2
ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira
alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi laki
mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo na
kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua
zaidi za kisheria.
CREDIT: GPL
0 comments:
Post a Comment