Hivi Ndivyo basi la New Force linavyo onekana kwa Mbele Baada ya kupata ajali
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akiwa anatembelea eneo ambapo ajali hiyo ilitokea
Askari wa Usalama wa barabarani wakiwa eneo la tukio
Basi la New Force upande wa Mbele
Miili ya watu wawili waliofariki katika ajali hiyo
Kazi ya kuwaokoa ndani ya basi la New Force inaendelea
Baadhi ya watu wakiwa wameokiolewa
Majeruhi
Mashuhuda
Basi la New Force
Mmoja wa Mashuhuda akilia kwa uchungu
WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE
WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI
YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA
KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, BARABARA KUU YA
MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA BASI HILO
LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954 AMH
AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA
MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA
KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI,
AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA
KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
CREDIT : MBEYA YETU
0 comments:
Post a Comment