Friday, 20 June 2014

TUMWONE HURUMA:WAKIMBIWA NA MUME WAKE KISA UGONJWA WA SARATANI

...

INASIKITISHA! Mama mmoja  mkazi Karagwe mkoani Kagera, Josephine
 Domisian (34) ametelekezwa na mumewe aitwaye Dominic baada  ya kupatwa 
na ugonjwa wa  saratani ya kizazi miaka mitatu iliyopita.


 Akizungumza kwa uchungu akiwa katika hospitali ya magonjwa ya Saratani ya
 Ocean Road, jijini Dar mama huyo alisema awali mumewe alikuwa akimnyanyapaa
 kwa kumnyima msaada hata wa chakula, hali iliyosababisha wanakijiji wenzake 
kumsaidia fedha za usafiri wa kumpeleka Dar kwa ajili ya matibabu. “Nilisaidiwa 
 kiasi cha shilingi 150,000 na kufanikiwa kufika hospitalini. Kule nilimuacha mume
 wangu na wanangu wanne, lakini nimepewa taarifa kwamba mume wangu
 amewaacha watoto, sasa wanalelewa na majirani na yeye ameoa mke mwingine.


Josephine Domisian akiwa amejipumzisha katika hospitali hiyo.
 “Kwa sasa napata msaada kutoka kwa wagonjwa  wenzangu au kutoka kwa ndugu wa wagonjwa ndiyo wananipa chakula na baadhi ya matumizi hapa hospitalini. Kule nyumbani wanangu wanaishi kama yatima, hawaendi shuleni maana hakuna mtu wa kuwapa huduma muhimu kama sare na vitu vingine.“Hapa hospitalini nimeruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yangu kuwa nzuri kidogo, natakiwa kuja tena baada ya miezi sita lakini sina hata nauli ya kunifikisha kwetu na sijui nitapata wapi. Nawaomba Watanzania wanisaidie nauli ili nikawaone wanangu, naumia sana,” alisema mama huyo kwa huzuni.

Afisa uhusiano wa taasisi  hiyo, Nicolas Mshana amethibitisha kuruhusiwa kwa mama huyo. Yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana na Josephine kwa kutumia simu namba
0757 106143. 
-GPL
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger