Jeshi
la Polisi limethibisha kupokea tuhuma za ubakaji dhidi ya mume wa
mwimbaji wa injili Flora Mbasha anayefahamika kwa jina la Emmanuel
Mbasha.
Akiongea
na Tovuti ya Times Fm, kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala,
Marietha Minangi ameeleza kuwa jeshi hilo limepokea tuhuma hizo kutoka
kwa mlalamikaji ambaye ni binti mwenye umri wa miaka 17 na kwamba binti
huyo alifika katika kituo cha polisi akiwa na ndugu zake.
“Taarifa
zimepokelewa na zinachunguzwa. Taarifa zilizokuja ni za kubaka sasa
tunazichunguza tufike mwisho tujue ni nini.” Kamanda Minangi ameimbia
tovuti ya Times Fm.
Ameeleza
kuwa baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mlalamikaji polisi
walienda nyumbani kwake ambapo hawakumkuta yeye na mkewe na kwamba hadi
sasa hawajapatikana.
Tovuti
ya Times Fm ilitaka kupata ufafanuzi kuhusu uhusiano uliopo kati ya
mlalamikaji na mtuhumiwa kwani taarifa za awali zinadai kuwa ni shemeji
wa mtuhumiwa.
“Hayo
yote yanachunguzwa, mimi siwezi kusema ni shemeji yake kabla
hatujafikia mwisho wa uchunguzi. Tutakapofikia mwisho wa uchunguzi ndipo
tutakapoweza kusema wana mahusiano gani.” Kamanda Minangi ameeleza.
0 comments:
Post a Comment