Sunday, 1 June 2014

OMMY DIMPOZI APATA KIMWANA-KICHEKI HAPA

...

OOmmy Dimpoz amefunguka na kudai kuwa mitandao ya kijamii imempa mke mchumba.
915559_591874717578603_1984267566_n
Mrembo wa Ommy Dimpoz


Ommy amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa yeye na msichana huyo waliweza kukaa kwa muda wa mwaka mmoja wakichati bila kuonana.
“Social network zilisaidia kutuunganisha lakini matokeo yake mpaka tukaja kuonana. Mpaka nikaja kwenye tour tukaonana, si unajua kuna zile mzee unashangaa ma Instagram mtoto ka like picha kama tisini hivi, halafu ukichekecha unaona mbona kama umechorwaee ,bahati nzuri ilipoanzishwa instamessage kwahiyo kama unajiiba hivi. 

Ni Mtanzania, mpaka kuonana ilichukua kama mwaka, tumechat tumechat mpaka ikafikia time, sina haraka kwanini niwe na haraka, kuamiana kunakuja automatically,” alisema.

“Unajua mambo ya mapenzi Mungu mwenyewe ndio anajua, pengine wengine anaweza wewe ukawa muuza mkaa demu akaja kununua mkaa. 

Lakini lile kopo unavyolishika kimachejo wakati wa kupima yeye anapenda ule upimaji wako, kwahiyo kuna kitu kama hivyo haijalisha mnakutana wapi, ikiwa tu mmewekea mipaka yenu, masharti hivi na hivi maisha yenu yanaenda.”
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger