Sunday, 1 June 2014

MASANJA NA DIAMOND WASHAMBULIWA NA MASHABIKI,WASHINDWA KUTOA POLE MISIBA 3 BONGO

...

Ukiingia Instagram leo utakutana na post nyingi za R.I.P George Tyson katika akaunti za wasanii wengi wa bongo movie na wa muziki, pamoja na wadau mbalimbali wa burudani, ingawa hakuna dalili za huzuni katika akaunti ya Diamond na Masanja zaidi ya picha za bata nchini Marekani.

Masanja3
Mashabiki wa muigizaji wa Ze comedy, Masanja Mkandamizaji pamoja mashabiki wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz wameshindwa kuvumilia kuona hawajihusishi hata kwa kutoa pole katika kipindi cha majonzi ya misiba mitatu iliyoongozana wiki mbili zilizopita katika akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Ndani ya wiki mbili zilizopita tasnia ya burudani Tanzania imepoteza watu watatu muhimu upande wa bongo movie, ambao ni muongozaji wa filamu Adam Kuambiana aliyefariki May 17, ukafuatia msiba wa muigizaji Rachel Haule aliyefariki May 26, na muongozaji wa filamu George Tyson aliyefariki jana May 30 kwa ajali ya gari.
masanja1
Chanzo cha mashabiki hao kuwashambulia Diamond na Masanja ambao wote wako Marekani kwa sasa kutokana na jinsi ambavyo wamekuwa wakipost picha za kula bata zaidi hata wakati ambao watu wana huzuni ukizingatia wao ni watu maarufu, pia ni wasanii na wanafuatiliwa na watu wengi kama kioo, pia misiba iliyotokea inawahusu pia sababu waliofariki ni wasanii wenzao.
masanja2
Katika akaunti za Instagram za Masanja na Diamond ndani ya wiki mbili hadi leo hakuna yeyote kati yao aliyepost kitu chochote kuhusu msiba wa Adam, Rachel wala Tyson, huenda ndio kilichowaudhi na kuamua kuwapa makavu live.
Masaa 11 yaliyopita Masanja amepost picha akiwa anataka kupanda ndege kuelekea North Carolina, na masaa 5 yaliyopita amepost picha akiwa amefika na kuandika ‘Asante Mungu North Carolina’s Safe!’


Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki wa Masanja:

angiellyicious – Hvii wewe unajua kama wasanii wenzako huku wana misiba au unakula raha tuu huko huna habari tena na kwenu!?? @mkandamizaji si uonyeshe japo kwa ku fake kuwa unahuzunika we ni mipicha ya raha tuuuu!!! 3h

sikudhanimtambo – Yaani huyu yeye ni mipicha ya batani tu,,,kasahau hata kuna kufa,,,wenzio wako misibani

rewardmassawe – Mimi Kila cku nawaambia Masanja ni POPOMPO kaz yake kupost pic zake za bata tu wenzako huku ni misiba tu bwege wewe au unazani wewe hutokufa

bintijuma11 – ila kweli jamani utasema askii taarifa za misiba hata pole za uongo huna kaka

bintijuma11- @dalila022 tatizo sio kupost picha za marehem we jiulize ndani ya hz wk mbili imetokea misiba mingapi na yeye muda wote anapost yuko happy tu hata kama aimuumi inabd awe soni kwa pindi mpendwa so kuturushia vipicha vyake vya bata 

sikudhanimtambo- Tunampenda but hata kama hajali mambo ya misiba azuge tu kuhuzunika,,,,au ye ataish milele mwenzetu

diamond usa
Baada ya Diamond kupost picha hii alfajiri ya leo na kuandika ‘Crazy Hunh…?’ hizi ni baadhi ya comment za mashabiki:

Kimatire- Ww dogo ulizaga kwanza hbr za nymbn cyo unatupia ma uchafu yako wkt wenzio wapo kwny maombolezo..punguza sifa

misspopote – Hivi huinag misiba au kwa vle n bongomovie nawe n bongofleva…..??inamaana wote hawakugusi @diamondplatnumz

kimatire – Hata mkimtetea lzm aambiwe”’sifa hazijengi’ huo muda wa kupost huo ‘uchafu”’angeutumia kutoa pole’kwa hli nitukaneni matusi yote”’jpo shabiki wake lkn muhmu kumwambia ukwel

hawamafixhbaby -Una habar na misiba unafany yko2 ujui kexho itakuaje platnumz ss 2nakupend lakin misiba unaipotezea cijaona hta pich yk moj una andik kuhus misiba pexa za kwak2 unasiaxh hp hp ndug watasi2mia kuwa na huruma kk nyang???????????
Hata hivyo baada ya madongo hayo, Diamond aliamua kuwa mwerevu kwa kufanya kile mashabiki wake walimtaka afanye kwa kuandika:
Najua tumekuwa tukipitia kipindi kigumu sana hivi karibuni.. kuondokewa na ndugu zetu ambao tunawapenda na kuwategemea kwenye sanaa na mambo mbalimbali.. kiukweli ni pigo na Pengo kubwa kwa Taifa… lakini skuzote tunaamini Sisi tuliwapenda ila Mwenyez mungu aliwapenda zaidi… Maombi yetu ndio yatakayo wasaidi walipo wapumzike kwa Amani….Mwenyez mungu azilaze roho zao mahala pema peponi Amin



Naye Masanja Mkandamizaji amejibu tuhuma hizo kwa kuandika:

Naona kuna watu wanahoji mbona siweki picha ya Misiba Inayotokea. JIBU
MAISHA NI MIPANGO NA MAAMUZI NILIAMUA SITAWEKA PICHA YA MSIBA WOWOTE ISTAGRAM KWA MAANA HAISAIDII CHOCHOTE, NILIFIWA NA DADA YANGU NA MDOGO WANGU WA MWISHO NA SIJAWAHI WEKA INSTA. NACHOJUA NI KWAMBA YANAPOTOKEA HAYA NI KUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,TENA SIO KUMSHUKURIA INSTA UNAMSHUKURU MOYONI WAKO. SO NIWAOMBE MLIOKUWA MNASUBIRI NIPOST SITAPOST NG’O!! NA KWA TAARIFA MSIBA WA ADAM NILIKUWEPO LIDAZ NA MCHANGO NIKATOA LKN SIKUWEKA PICHA ISTAGRAM. SO HUWA SIONGOZWI NA WATU KUFANYA KITU.
NA NILIACHAGA BAADA YA KWENDA KWENDA KWENYE MSIBA WA NGWEA MORO NIKAWEKA PICHA RAIA WAKAANZA OOOOH UNAUZA SURA. MALA MBONA SURA HAINA MAJONZI HEE SA MNATAKA NIJIUMBE MWENYE SURA YA MAJONZI ILI NIMKOSOE MUNGU ALIYENIUMBA HANDSOME JAMANI??? NEVER SITAWEKA PICHA ZA HIVYOOO INSTA. HAPA NI MACHAPIII YA UNAITEDI MPAKA NAVYORUDI NIKAWAPE POLE WAFIWA.
NADHANI KAMA ULINIFOLOOOOOO KUPATA UPDATE ZA MISIBA. U BETTER GO TO HELL. ETI KIOO CHA JAMIII(kwa ku bana pua moja na kidole) KIOO CHA JAMII CHA BABAKOOO. … #ChekilihotubaKamaLaMheshimiwaRais#
#HarafuNimeliwekaKwaHerufiKubwaa#
#UsichezeNaMimiKwenyeExplanesheniiiii#
#HahahahaaaNaonagaCommentZaPichaZaMisibaUtasikiaSaAmewekajeKopeMsibaniAmevaajeMiwaniAmefyokofyokomsibaniYaanWaliofeliLifeWanashidaaaaa#
#KumbukaNaongozwaNaRoho#
#Over#
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger