Tuesday, 17 June 2014

N/ WAZIRI KITWANGA ATEMBELEA BWAWA LA MTERA

...

2Mhandisi Mwandamizi masuala ya uendeshaji katika Bwawa la Mtera, Mhandisi Julius Chomora akimweleza Naibu Waziri Nishati  Mhe. Charles Kitwanga namna mtambo  wa uendeshaji unavyofanya kazi. Anayefuatia ni Mhandisi Nishati Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini Salum Inegeja. 3Naibu Waziri Nishati na Madini Mhe. Charles Kitwanga katikati akiongea jambo wakati Uongozi wa Bwawa ulipowasilisha  taarifa kuhusu Bwawa la Mtera. Anayefuatia kulia kwake ni Meneja Mwandamizi Kanda ya Kati Mhandisi Godwin Mzava na anayefuatia ni Meneja Uzalishaji TANESCO, Mhandisi Costa Rubagumwa. 4Kaimu Meneja wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Mtera, Mhandisi Steven akimwonesha Mhe. Charles Kitwanga moja ya “Transfoma ‘’ iliyopo katika eneo la Bwawa la Mtera.
……………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Mtera.
Naibu Waziri Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Mhe. Charles Kitwanga amefanya ziara ya kutembelea Bwawa la kuzalisha Umeme la Mtera mwishoni mwa wiki kwa lengo la kuangalia mwenendo wa maji katika bwawa hilo.  
Wakati akizungumza na watendaji wa Bwawa hilo, Kitwanga amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa Bwawa la Mtera linaendelea kuwa na kiasi cha maji ya kutosha wakati wote ili kuweza kuzalisha umeme wa kutosha.
“Lazima muhakikishe bwawa hili linakuwa na maji ya kutosha wakati wote. Hakikisheni kuwa vyanzo vya maji ya bwawa hili vinakuwa endelevu”. Amesisitiza Kitwanga.
Aidha, ameongeza kuwa, uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni muhimu kutokana na gharama zake kuwa nafuu ikilinganishwa na gharama za kuzalisha umeme unatokana na gesi au vyanzo vingine. Hivyo, amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao jirani na vyanzo vya maji kuhakikisha wanavilinda kwa ajili ya maendeleo na manufaa ya taifa.
Katika hatua nyingine amewataka watendaji hao kufikiria vyanzo vingine vya kuzalisha umeme mbali na gesi badala ya kusubiri rasilimali ya gesi pekee kuweza kuzalisha umeme.
“Tukumbuke gesi inaweza kuisha, lakini kuna vyanzo vingine vingi ambavyo vinaweza kwenda sambamba na gesi, lazima tuwe wabunifu”. Ameongeza.
Aidha ameeleza kuwa, wananchi wana matarajio makubwa na nishati ya umeme hivyo, amewataka watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuwatumikia watanzania huku wakitanguliza uzalendo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger