Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Mheshimiwa Chiku Gallawa atakuwa mgeni
rasmi katika shindano la kumsaka mrembo wa mkoa huo, Nice & Lovely
Miss Tanga 2014 siku ya jumamosi tarehe 21/06/2014, shindano ambalo
litafanyika Mkonge Hotel.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotions ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga amekubali kuwa mgeni rasmi, napia amepongeza maandalizi makubwa yaliyofanyika katika kuliandaa shindano hilo ambalo limekuwa gumzo katika jiji la Tanga.
“Tumedhamiria kulifanya shindano
hili kuwa na msisimko wa kipekee, na maandalizi yote yamekamilika kwa
aslimia mia moja nasasa tunasubiria siku ikfike ili kumpata mshindi,
alisema Irene.
Warembo wote 13 hivi sasa wapo kambini katika Hoteli ya
Tanga Beach Resort chini ya mwalimu wao Mariam Bandawe na wanaendelea
vizuri na mazoezi yao. Mshindi wa kwanza wa shindano hilo atazawadiwa
zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz ambalo tayari limeshapelekwa
mkoani Tanga karibu wiki tatu sasa.
0 comments:
Post a Comment