Tuesday, 17 June 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

...
 DSC00207MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GODFREY MMBENA (22) MKAZI WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYAAKIWA NOTI BANDIA 23 ZA TSHS 10,000/=.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 16.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUTWA NA NOTI ZA TSHS 10,000/= ZIPATAZO 23 SAWA NA TSHS 230,000/= ZIKIWA NA NAMBA BU-7282393 – NOTI 9, NAMBA BU-7282392 NOTI 5, NAMBA BU- 7282395 NOTI 5, NAMBA CK-1942919 NOTI 2, NAMBA AP 3412534 NOTI 1 NA NAMBA AP 3412537 NOTI 1.
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA MATAPELI HASA KATIKA MAENEO YA BIASHARA PIA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTANDAO WA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger