Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32) wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.Baada ya Monica Lutonja kufungua

walianza
kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza
fahamu.Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na
kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja
na wakaanza kumpiga hadi kumuua.Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph
Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa watuhumiwa
wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
0 comments:
Post a Comment