Mfanyakazi
wa ndani, miaka 14 mkazi wa kijiji cha Mdenge, Kata ya Likombe katika
Wilaya ya Mtwara, amebakwa na mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na
kumsababishia maumivu makali na kisha kutokomea kusikojulikana.
Akiongea
jana Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa
miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu
aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu
(42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani
humo.
Amebainisha
kuwa, mtoto wake alipata kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo
Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua
kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga
kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na
kukimbilia nyumbani kwao.
“Alivyopata
kazi anasema hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivyo hii ni mara ya
pili, usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 14, 2014 alimuingilia mtoto
wangu na alipomwambia atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa mtu yeyote
kwani atamfanya kama mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.
“Nimemkuta
yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo
mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi” alisema mama wa mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa
nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele
alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na
usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka
alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa
maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.
FikraPevu
ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye
hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila kupokelewa,
huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo wakidai
hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment