UBABE! Tofauti na inavyoaminika na wengi kuwa mfumaniwaji huwa mpole, kibao kimebadilika, mfanyakazi wa ndani aliyejulikana kwa jina la Niachie amegeuka mbogo na kumchoma bisibisi bosi wake, Amina ‘Mama Zai’ aliyemfumania akiwa na mumewe aitwaye Amri.
Amina au Mama Zai akionyesha jeraha alilojeruhiwa na mfanyakazi wake wa ndani baada ya kumfumania akiwa na mumewe.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Mbagala jijini Dar ambako
mama Zai alimwekea mtego mfanyakazi wake huyo wa ndani baada ya kubaini
kuwa alikuwa akitembea na mumewe wakati yeye akiwa kazini.ISHU ILIVYOANZA
Akizungumza na paparazi wa kitengo maalum cha kufichua maovu (OFM) siku mbili kabla ya tukio, mama Zai alidai kuwa mumewe ana kawaida ya kufanya mapenzi na mfanyakazi wao wa ndani wakati yeye akiwa kazini hivyo akaandaa mtego ili kukomesha tabia hiyo.
KUMBE NI NESI
Mama Zai alizidi kumwaga data kuwa, yeye ni nesi katika hospitali moja ya mtu binafsi iliyoko Jangwani jijini Dar hivyo akiwa zamu ya usiku, mumewe hutumia mwanya huo kubanjuka na hausigeli.
“Ananivizia nikitoka tu na akijua nimeshafika mbali, anaingia chumbani kwa hausigeli na kuvunja naye amri ya sita,” alidai mama huyo.
MTEGO WANASA
Mama huyo alisema ili kufanikisha zoezi la kumnasa mumewe, alijifanya anakwenda zamu ya usiku kisha akajifungia stoo ili aweze kufanya fumanizi matata.
Kama kawa, OFM ilitia timu nyumbani kwa mama huyo ikiwa kamili na zana zake, ikakita kambi katika baa moja iliyo jirani na nyumba hiyo na ilipofika saa tano usiku, ishu ikatiki, baba Zai aliingia katika chumba cha mfanyakazi huyo kwa lengo la ‘kuharibu’.
'MISS IN ACTION’
Wakati makamanda wa OFM wakiwa ‘wanaseti’ kamera zao huku wakisubiri polisi na mwenyekiti wa serikali za mtaa wafike eneo hilo, mama Zai alivamia chumba hicho (alihofia baba atamaliza mchezo) na purukushani ya nguvu ikaanza.
Katika harakati za kujinasua katika kipigo cha bosi wake, hausigeli huyo aliokota bisibisi na kumchoma mama mwenye nyumba shingoni kisha kutimua mbio huku mume naye akiingia mitini.
0 comments:
Post a Comment