Friday, 6 June 2014

TANGAZO MUHIMU KUHUSU MAFUNZO YA VIJANA MUJIBU WA SHERIA 2014

...
TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWATANGAZIA VIJANA WANAOJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA KWANZA JUNI 2014 KURIPOTI MAKAMBI WALIYOPANGIWA HARAKA IWEZEKANAVYO KWANI MAFUNZO YATAANZA RASMI TAREHE 09 JUNI 2014.
AIDHA, LINAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA MANENO (SMS) KATIKA SIMU ZA VIGANJANI KWAMBA WALIORIPOTI KAMBI YA MAKUTUPORA DODOMA WALIPOKELEWA NA KUTESWA, HAWAKULALA WALA KULA CHAKULA HUKU KIJANA MMOJA TOKA SHULE YA SEKONDARI PUGU AKIVUNJWA MGUU KWA MATESO. YOTE YALIYOSEMWA SIO KWELI BALI NI MANENO YA UZUSHI TU...

IFAHAMIKE TAARIFA HIZO SI ZA KWELI, HUU NI UPOTOSHAJI KWA UMMA WA WATANZANIA, HADI TAREHE 02 JUNI 2014 HAKUNA KIJANA ALIYERIPOTI KATIKA KAMBI YA MAKUTUPORA ANAYETOKA SHULE YA SEKONDARI PUGU, WALA HAKUNA ALIYEVUNJIKA MGUU, KUCHELEWESHWA KUPATA HUDUMA YA CHAKULA WALA KUTOKULALA. HII NI KWASABABU HAKUNA MAFUNZO YALIYOKWISHA ANZA, KINACHOFANYIKA NI MAPOKEZI YA VIJANA TU.
JKT LINALAANI KITENDO HICHO, LINAFUATILIA CHANZO HICHO NA KIJANA AMA MTU YEYEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUWA NDIYE ALIYEPOTOSHA VIJJANA NA UMMA WA TANZANIA, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
JTK INAWAKUMBUSHA VIJANA NA WATANZANIA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA MITANDAO HASA KWA TAARIFA ZINAZOHUSISHA JESHI.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MAKAO MAKUU YA JKT
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger