DIAMOND PLATNUMZ HALALI. PAMOJA NA MAFANIKIO MAKUBWA ANAYOENDELEA KUYAPATA, STAA HUYO ANAZIDI KUJITENGENEZA CONNECTION KALI ZA KIMATAIFA.
Picha ya juu: Diamond akiwa na Kevin Liles, meneja wa Trey Songz, Big Sean, Estelle na wasanii wengine
Katika kile kinachoonekana kuwa ni mazungumzo ya mwanzo wa safari ya kuelekea kuanza kufanya collabo na wasanii wa Marekani, Diamond amekutana na meneja wa Trey Songz, Big Sean na wasanii wengine wakubwa, Kevin Liles.
Mmoja wa watu waliopo kwenye timu ya Diamond, Salam wa SK Entertainment, ameshare picha nay a Diamond akiwa na Kevin Liles na kuandika: “Don’t Ask Me Whats Next…. Please 2 Days to go… VOTE FOR @diamondplatnumz for MTV MAMA Awards BEST COLLABORATION AND BEST MALE.”
Kevin akiwa na Jay Z
Kevin Liles alikuwa rais wa Def Jam Recordings na makamu mkuu wa rais wa The Island Def Jam Music Groupkuanzia mwaka 1999 hadi 2004.
Kevin na Trey Songz
Pia aliwahi kufanya kazi kama makamu mkuu wa rais wa Warner Music Group kabla ya kuacha na kuwa mjasiriamali. Ana kampuni ya menejimenti iitwayo KWL Management.
0 comments:
Post a Comment