MTU mmoja
anayetuhumiwa kwa wizi wa ng’ombe na ndama wake, mwishoni mwa wiki
iliyopita alipata kipigo cha kufa mtu na baadaye kuchomwa moto, lakini
katika hali isiyo ya kawaida, hakuweza kufariki ‘kugoma kufa’ hadi
polisi walipotokea na kunusuru maisha yake.
Mtuhumiwa
wa wizi wa ng'ombe akiwa kwenye majani yaliyotumika kumchochea moto
mara baada ya kupata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa wamiliki wa ng'ombe
hao huko Mwasanga, Ivumwe jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Blog ya Mbeya yetu, tukio
hilo lilitokea Mwasanga, Ivumwe jijini Mbeya kufuatia kuibiwa kwa
wanyama hao usiku nyumbani kwa Kongoro Mwakitalima, ambaye ni mkazi wa
Isyesye Kata ya Ilomba.
Ilidaiwa baada ya mwizi huyo kuwachukua
wanyama hao, mtu huyo aliwapa taarifa majirani zake, ambao asubuhi na
mapema walijihimu na kuanza kuwatafuta ambapo baada ya kufika eneo la
Ivumwe walikutana na mwendesha bodaboda ambaye aliwaambia alikutana na
mtu akiwa anaswaga mifugo hiyo.
Walipoambiwa hivyo, wananchi hao
wakitumia bodaboda, walimfukuzia mtu huyo na kufanikiwa kumkuta katika
eneo la Mwasanga relini akiwa na ng’ombe hao.
Shuhuda alisema wananchi walikusanyika
na kuanza kumshushia kipigo kikali, lakini licha ya uzito wa mkong’oto,
bado mtuhumiwa huyo alionekana kuwa ngangari ndipo waliamua kumchoma
moto.
Hata hivyo, licha ya moto huo, bado mtu huyo hakuweza kukata roho hadi askari polisi walipofika eneo hilo na kumchukua.
Hata hivyo, licha ya moto huo, bado mtu huyo hakuweza kukata roho hadi askari polisi walipofika eneo hilo na kumchukua.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo alikuwa hai au la!
0 comments:
Post a Comment