HATIMAYE familia
ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius
Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata,
imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.
Akizungumza na Uwazi, mwishoni mwa wiki
iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa
na daktari aliyemfanyia uchunguzi inamaliza utata na minong’ono yote
inayoendelea chuoni.
Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo
cha Sekabenga kimetokana na mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa
sawa, jambo lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia.
“Daktari amesema kwamba mishipa ya damu
haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa
sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu,” alisema
Mwigune.
Uwazi lilifunga safari hadi chuoni na
kuzungumza na baadhi ya wanafunzi ambao walionyesha wasiwasi kuwa huenda
marehemu aliamua kujiua kwa sumu kwa maelezo kuwa, siku chache kabla ya
kifo chake alionekana mwenye mawazo mengi.
“Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa
na jambo zito linalomsumbua ndiyo maana unasikia wanafunzi wengi hapa
chuoni wanahusisha kifo chake na sumu,” alisema denti mmoja kwa sharti
la kutotajwa jina lake.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwa familia
inayonukuu ripoti ya daktari inaziba minong’ono yote kwa kuwa haionyeshi
mahali popote kuwa marehemu alijiua kwa sumu.
Mwili wa Sekabenga ukiingizwa kwenye gari.
Marehemu Sekabenga alikuwa mwaka wa pili
chuoni hapo akichukua Shahada ya Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili
wake umesafirishwa Jumamosi Mei 31, mwaka huu kwenda mkoani Mbeya kwa
maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana Jumatatu.
Gazeti hili linatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
0 comments:
Post a Comment